• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • CIT yaleta neema ya ajira  zaidi ya 1,000

    (GMT+08:00) 2019-05-17 18:56:37
    Shirika la Kimataifa la Compasion International (CIT), kupitia ushirika wa makanisa wenza nchini Tanzania limetoa neema ya ajira zaidi ya 1,300 katika miradi yake mbalimbali inayotekeleza nchini humo kama njia mojawapo ya kuunga mkono juhudi za Rais Dk. John Magufuli kupunguza changamoto hiyo.

    Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Taifa wa CIT, Agness Hotay, shirika hilo limefanikiwa kutekeleza ndoto yake ya kushiriki katika kupunguza pengo la ajira kwa kutengeneza ajira hizo na kuchangia pato la taifa.

    Aliongeza kuwa mpaka sasa huduma yao ya kuwakomboa watu masikini imewafikia vijana 135,750, lakini pia kupitia makanisa wenza wametoa ajira zaidi ya 1,300 hivyo kushiriki katika kuondoa uhaba wa ajira kwa kutengeneza ajira na kuchangia pato la taifa.

    Shirika hilo liko katika mikoa 19 ya Tanzania Bara ambayo ni Arusha, Dar es Salaam, Kigoma, Manyara, Pwani, Morogoro, Iringa, Dodoma, Kilimanjaro, Singida, Shinyanga,Mwanza, Mara, Tabora, Lindi, Geita, Mtwara, Simiyu na Kagera.

    Miradi iliyoibuliwa na kufadhiliwa na Shirika hilo katika Wilaya ya Siha ni wa ufugaji wa kuku chotara ambao mwaka 2017 unaendeshwa na kinamama wa huduma ya kunusuru pamoja na kanisa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako