• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Vijana Tanzania watakiwa kutumia mitandao kwa manufaa yao ya kiuchumi

    (GMT+08:00) 2019-05-17 19:03:18

    Vijana nchini Tanzania wametakiwa kutumia mitandao ya kijamii kujiletelea mafanikio kiuchumi.

    Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe, Jokate Mwegelo, alitoa ushauri huo wakati wa mdahalo wa kujadili changamoto mbalimbali zinazomkabili mtoto wa kike na mwanamke katika Siku ya Familia iliyoandaliwa na Shirika la Plan International nchini.

    Mwegelo alisema vijana wengi kwa sasa wanatumia mitandao ya kijamii, lakini hawaitumii kwa usahihi kujiletea maendeleo ya kiuchumi na elimu badala yake wanaitumia kusambaza habari za uongo na umbea.

    Alisema vijana wakishikamana na kutumia mitandao vizuri kwa kujadili masuala ya msingi kama elimu na jinsi ya kujikwamua kiuchumi, wanaweza kufika mbali na kupiga hatua kimaendeleo.

    Alisema mitandao ya kijamii imeonyesha mafanikio makubwa katika kampeni ya 'Tokomeza Ziro' wilayani mwake kwa kuwa amepiga hatua katika kutokomeza ziro mashuleni wilayani Kisarawe.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako