• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Msomi wa Marekani asema nchi hiyo inaichukulia China kama chanzo cha masuala yote

    (GMT+08:00) 2019-05-17 20:43:51

    Mtafiti wa juu wa taasisi ya utafiti wa mambo ya dunia ya Chuo Kikuu cha Yale cha Marekani Bw. Stephen Roach, ametoa makala akisema wanasiasa wa Marekani wamepokea wazo lisilo sahihi kuhusu China, na kuichukulia China kama chanzo cha masuala yote yanayoisumbua Marekani.

    Makala hiyo inasema wanasiasa wa vyama vya Republican na Democrat vya Marekani wameafikiana kuchukulia China kama chanzo cha matatizo yote, lakini hali hii itasababisha taabu kubwa. Kwa mfano wa suala la biashara, Marekani ina pengo la biashara na nchi 102 duniani, kutokana na upungufu wa akiba ya wamarekani. Lakini ikilinganishwa na hatua halisi ya kutatua suala hilo, kuichukulia China kama chanzo cha matatizo ni rahisi zaidi.

    Makala hiyo inasema, serikali ya Marekani haichambui suala la China kwa makini na kufikia hitimisho lisilo sahihi, huku wamarekani wengi wakiamini hitimisho hilo bila kujali ukweli.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako