• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tanzania inapanga kufungua kituo cha matibabu ya saratani kwenye nyanda za juu kusini

    (GMT+08:00) 2019-05-18 17:18:51

    Serikali ya Tanzania imesema inapanga kufungua hospitali ya matibabu ya saratani katika eneo la nyanda za juu kusini, yenye mikoa sita ya Katavi, Rukwa, Mbeya, Njombe, Iringa na Ruvuma.

    Naibu waziri wa Afya wa Tanzania Bw. Fausitine Ndungulile amesema mjini Dodoma kuwa, kufunguliwa kwa hospitali hiyo kutapunguza idadi ya wagonjwa wanaosafiri kwenda Dar es salaam kutafuta matibabu.

    Amesema matibabu ya magonjwa yasiyo ya kuambukizwa ikiwa ni pamoja na saratani ni gharama sana, na idadi ya wagonjwa wa ugonjwa huo wamekuwa wakiongezeka.

    Mbali na hatua hiyo Bw. Ndungulile amesema serikali inapanga kuanzisha kampeni ya kuinua mwako wa wananchi ili kuwafanya wananchi wachukue hatua za kujikinga.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako