• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kampuni ya China yazindua mradi wa maji kwa ajili ya jamii za kusini magharibi mwa Kenya

    (GMT+08:00) 2019-05-18 17:19:09

    Kiwanda cha utengenezaji wa malumalu cha China KEDA, jana kilizindua mradi wa kusambaza maji ili kuzisaidia jamii za kaunti ya Kajiado kusini magharibi mwa Kenya.

    Balozi wa China nchini Kenya Bw. Wu Peng amesema kwenye sherehe ya uzinduzi wa mradi huo unaofadhiliwa na kampuni ya KEDA, ikiwa ni sehemu ya uwajibikaji wa kampuni kwa jamii, kuwa anapongeza miradi kama hiyo na kutumai kuwa kampuni ya KEDA na kampuni nyingine za China zitafanya kazi zaidi, na sio kama tu zitasafirisha teknolojia na kuleta maendeleo, na kuonyesha urafiki kutoka kwa jumuiya ya wafanyabiashara wa China kwa wenyeji.

    Naibu gavana wa kaunti ya Kajiado Bw. Martin Moshisho amesema mradi huo umekuja kwa wakati mwafaka kwa kuwa kaunti hiyo inakabiliwa na uhaba mkubwa wa maji, na ni asilimia 36 tu ya wakazi wanapata maji.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako