• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • "Marekani inaihitaji Huawei"-New York Times

    (GMT+08:00) 2019-05-18 17:28:56

    Gazeti la Marekani New York Times la Marekani limechapisha makala ya naibu mkrugenzi mkuu wa kampuni ya Huawei ya China Bibi Chen Lifang, ikisema Marekani inaihitaji Huawei, na kukosoa amri ya zuio dhidi ya Huawei.

    Katika makala hiyo yaitwayo "Marekani inaihitaji Huawei", Bibi Chen amesema kitendo cha kupiga marufuku uuzaji wa vifaa vya kampuni ya Huawei nchini Marekani kitaifanya Marekani ipoteze maelfu ya nafasi za ajira, na kuongeza gharama ya uendeshaji kwa makampuni ya mawasiliano ya simu yanayotumia vifaa vya Huawei. Mbali na hayo, Huawei ikiwa ni kiongozi kwenye sekta ya teknolojia ya 5G, amri hiyo ya zuio itazuia Marekani kwenda na wakati na kuharibu uchumi wake.

    Amesisitiza kuwa kitendo hicho hakiwezi kutimiza lengo la kuimarisha usalama wa mtandao wake wa internet wa kidigitali. Marekani inapaswa kutunga kanuni za pande zote juu ya usimamizi wa hatari, kama mkakati ulivyowekwa na wizara yake ya usalama wa ndani mwaka jana. Serikali ya Marekani inatakiwa kuacha zuio hilo, na balada yake kuanzisha utaratibu wa udhibiti wa hatari,ili kutathimini na kulinda usalama wa mtandao nchini Marekani.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako