• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Waziri wa mambo ya nje wa China akutana na mwenzake wa Iran

    (GMT+08:00) 2019-05-18 17:58:00

    Waziri wa mambo ya nje wa China Bw. Wang Yi amekutana na mwenzake wa Iran Bw. Mohammad Javad Zarif hapa Beijing, na kusema China na Iran ni wenzi kamili wa kimkakati, nchi hizo mbili zinahitaji kuimarisha mawasiliano, na China inalinda makubaliano ya nyuklia ya Iran, na kulinda mamlaka ya Umoja wa Mataifa na kanuni ya kimsingi ya mahusiano ya kimataifa.

    Bw. Zarif amesema Iran inapenda kuimarisha uratibu wa pande mbili na pande nyingi, kuimarisha ushirikiano kati ya nchi hizo mbili kwa kujenga kwa pamoja "Ukanda Mmoja, Njia Moja".

    Pande hizo mbili pia zimebadilishana maoni kuhusu masuala ya Afghanistan, Syria na hali ya Asia Magharibi na Afrika Kaskazini.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako