• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Waziri mkuu wa Japan Shinzo Abe akutana na mjumbe wa kamati wa idara ya siasa ya Chama cha Kikomunisti cha China Yang Jiechi

    (GMT+08:00) 2019-05-18 17:58:33
    Waziri mkuu wa Japan Bw. Shinzo Abe amekutana na mjumbe wa kamati wa idara ya siasa ya Chama cha Kikomunisti cha China Bw. Yang Jiechi.

    Bw. Yang amesema China inaunga mkono Japan kuwa mwenyeji wa mkutano wa viongozi wa G20 huko Osaka, ili kuongeza imani na matarajio ya jumuiya ya kimataifa na kuleta matumaini zaidi katika maendeleo ya uchumi wa dunia.

    Bw. Shinzo Abe amesema anatarajia kukutana na rais Xi Jinping wa China mjini Osaka ili kuhimiza uhusiano na kufungua zama mpya ya uhusiano kati ya nchi hizo mbili.

    Bw. Yang amefanya ziara nchini Japan kutokana na mwaliko wa mkuu wa idara ya ulinzi wa usalama wa kitaifa ya Japan Bw. Shotaro Yachi, na kuongoza mazungumzo ya sita ya siasa ya juu kwa pamoja. Wakati wa ziara yake, Bw. Yang amekutana na waziri wa mambo ya nje wa Japan Bw. Taro Kono, na kiongozi wa baraza la serikali Bw. Yoshihide Suga.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako