• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mkutano wa diaspora ya afrika wanaoishi nchini China wafanyika Beijing

    (GMT+08:00) 2019-05-19 17:34:36

    Mkutano wa waafrika wanaoishi hapa China umefanyika leo hapa Beijing, ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 56 ya Umoja wa Afrika, na kuhudhuriwa na mabalozi mbalimbali wa Afrika nchini China, akiwemo balozi wa Rwanda, Malawi, Cape Verde na mwakilishi wa Umoja wa Afrika nchini China.

    Akiongea kwenye mkutano huo, mwakilishi wa kudumu wa Umoja wa Afrika nchini China Bw. Osman, amehimiza waafrika wanaoishi China kujifunza utamaduni na mambo yanayoweza kuhimiza maendeleo nyumbani. Balozi wa Rwanda nchini China amewataka waafrika wanaoishi hapa China kuwa mfano mzuri na kufanya bidii kwenye maeneo walipo.

    Waafrika wote wanaoishi China wamekumbushwa sio tu kuwasaidia watu walioko Afrika kuifahamu vizuri China na wachina, bali pia kuhimiza maendeleo ya uhusiano kati ya China na Afrika, na kutoa mchango kwa maendeleo ya Afrika.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako