• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mkutano wa mawaziri wa APEC wasisitiza kulinda mfumo wa biashara ya pande nyingi

    (GMT+08:00) 2019-05-19 18:42:47

    Mkutano wa 25 wa biashara wa mawaziri wa Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiuchumi ya Asia na Pasifiki (APEC) umefungwa jana huko Vina del Mar. Taarifa ya pamoja iliyotolewa baada ya mkutano huo imesisitiza kulinda mfumo wa biashara ya pande nyingi.

    Taarifa hiyo imesifu mchango uliotolewa na Shirika la Biashara Duniani (WTO) kwa biashara ya dunia na kukubali kuchukua hatua zinazohitajika kuboresha utendaji wa WTO.

    Msaidizi wa waziri wa biashara wa China anayemwakilisha waziri wake Bw. Li Chenggang amesema kuwa taarifa hiyo inaonyesha maoni ya nchi wanachama wa APEC kuhusu mfumo wa biashara ya pande nyingi na msimamo kuhusu kulinda kanuni za Shirika la Biashara Duniani.

    Habari zaidi zinasema mkutano usio rasmi wa viongozi wa APEC utafanyika mwezi Novemba huko Chile.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako