• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Ukuaji imara wa uchumi wa China watoa uungaji mkono katika kutuliza soko la fedha za kigeni

    (GMT+08:00) 2019-05-20 08:25:56

    Naibu mkuu wa Benki Kuu ya China na mkurugenzi wa Idara kuu ya usimamizi wa fedha za kigeni Bw. Pan Gongsheng amesema, ukuaji imara wa uchumi wa China umetoa uungaji mkono katika kutuliza soko la fedha za kigeni na kudumisha kiwango cha ubadilishaji wa RMB.

    Amesema China ina msingi, imani na uwezo wa kudumisha utulivu wa soko la fedha za kigeni, na kudumisha kiwango cha ubadilishaji wa sarafu ya China RMB. Pia amesema, hivi sasa uchumi wa China unakua kwa utulivu, vigezo vikuu vyote viko kwenye viwango vinavyofaa, na hali ya jumla ya uchumi ina mwelekeo mzuri.

    Bw. Pan amesisitiza kuwa China itaendelea kufungua mlango katika sekta ya fedha, kuimarisha mageuzi ya usimamizi wa fedha za kigeni, kulinda kihalisi maslahi halali ya wawekezaji wa ndani na wa nje, na kuendelea kuboresha mazingira ya uwezekaji nchini China.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako