• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wataalamu wa China waona kuwa Marekani kupaka matope China katika suala la ulinzi wa hakimiliki ya ubunifu kwa makusudio ya kisiasa

    (GMT+08:00) 2019-05-20 17:23:21

    Tangu mgogoro wa kibiashara kati ya China na Marekani ulipotokea, Marekani imekuwa ikitoa kauli zisizo na ukweli kuhusu China ili kukidhi mahitaji yake. Wataalamu wa China wanaona kuwa vitendo hivyo vya Marekani vimepotosha ukweli wa mambo ambavyo vina makusudio ya kisiasa.

    Naibu mkuu wa Kitivo cha hakimiliki ya ubunifu katika Chuo Kikuu cha Beijing Bibi. Zhang Ping ameshughulikia suala la ulinzi wa hakimiliki ya ubunifu kati ya China na Marekani kwa miongo kadhaa. Anasema takwimu zimeonesha kuwa, Marekani imekuwa ikitoza gharama kubwa za idhini ya hakimiliki ya ubunifu, huku ikipuuza faida ilizopata katika sekta hiyo. Anasema:

    "Kampuni ya utafiti wa TEHAMA ya Qualcomm ya Marekani imesaini makubaliano yenye thamani ya dola za kimarekani milioni kadhaa na Kampuni ya China Unicom. Lakini thamani ya biashara kati ya nchi hizo mbili haihusishi gharama hizo, kwani zimehesabiwa kwa njia ya gharama za kibali cha hakimiliki ya ubunifu."

    Mwaka 2016 China iliilipa Marekani dola bilioni 7.96 kwa matumizi ya hakimiliki ya ubunifu, kiasi ambacho kinashika robo ya fedha ya jumla zinazotozwa na Marekani, hali ambayo imeonesha kuwa ulinzi wenye ufanisi wa China wa hakimiliki ya ubunifu umeziletea kampuni za Marekani faida kubwa, lakini thamani hiyo imepuuzwa na Marekani.

    Katika miaka miongo kadhaa iliyopita, gharama zinazotolewa na China kutokana na matumizi ya hakimiliki za nchi za nje zimeongezeka kwa mara nne, na zilifikia dola za kimarekani bilioni 35.8 katika mwaka 2018, na kushika nafasi ya nne duniani. Profesa wa taasisi ya biashara kwenye Chuo Kikuu cha Umma cha China Bw. Xu Jiabin anasema:

    "Kampuni ya Apple imebakiza utaratibu wake wa teknolojia wa utengenezaji nchini China, kutokana na kwamba China imelinda vizuri hakimiliki yake ya ubunifu, na pia kampuni ya Apple. Kama China si nchi inayoweza kulinda vizuri hakimiliki ya ubunifu, inawezaje kuzivutia kampuni hizo nyingi za kimataifa kuja ili kutafuta ulinzi wa hakimiliki ya ubunifu?"

    Takwimu hizo vilevile zimeonesha kuwa, China imeanzisha utaratibu kamili wa kisheria tena za kiwango cha juu za hakimiliki ya ubunifu, kuzidi kuimarisha sheria katika sekta hiyo, na kuwa nchi inayoshughulikia kesi nyingi zaidi katika sekta hiyo duniani. Wataalamu wanaona kuwa, madai ya Marekani kwamba China iliiba hakimiliki ya ubunifu ni kitendo chenye makusudio ya kisiasa. Na maendeleo yaliyopatikana na China katika ubunifu wa sayansi na teknolojia, na uheshimu na ulinzi wake katika sekta hiyo zimekubaliwa na watu duniani.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako