• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kaunti kutwaa usimamizi wa kiwanda cha sukari cha Mumias

    (GMT+08:00) 2019-05-20 18:55:27
    Hali ya matumaini imerejea miongoni mwa wakulima wa miwa katika eneo la Mumias, Kaunti ya Kakamega, baada ya serikali ya kaunti hiyo kutangaza kuwa itachukuwa usimamizi wa shughuli za kiwanda cha Mumias Sugar.

    Gavana Wycliffe Oparanya alisema kuwa serikali yake itachukua usimamizi huo kutoka kwa bodi ya sasa ya wakurugenzi.

    Bw Oparanya alisema kuwa alifanya uamuzi huo baada ya bodi hiyo kutoa pendekezo la kukodishwa kwa baadhi ya mali ya kiwanda hicho kama maeneo ya kuzalishia maji na umeme, uwanja wa mchezo wa gofu, shule, nyumba zaidi ya 2,500 na chumba cha kuwapokea wageni.

    Akizungumza katika kikao maalum cha wadau katika mkahawa mmoja mnamo Ijumaa, Bw Oparanya alisema kuwa matumaini yake ni kuona kiwanda hicho kikirejelea shughuli zake kabla ya kumalizika kipindi chake kama gavana. Baadhi ya masuala yaliyopitishwa ni kuwa serikali ya kaunti inapaswa kubuni kundi maalum kusimamia shughuli za kiwanda hicho na hakuna jambo au uuzaji wowote wa mali utakaofanywa bila kumhusisha gavana na serikali yake. Mkutano huo pia ulipitisha kuwa kiwanda hicho kinapaswa kushirikiana na serikali kwa ustawishaji wa miwa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako