• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Asilimia ya bidhaa kutoka Rwanda kuja Uganda yapungua mno.

    (GMT+08:00) 2019-05-20 18:57:37
    Mzozo wa mpaka kati ya Uganda na Rwanda unaathiri biashara kati ya mataifa haya mawili. Kwa mujibu wa ripoti ya mwezi Machi iliyotolewa na benki ya Uganda, bidhaa zinazoagizwa kutoka Rwanda kuingia Uganda, zilipungua sana mwezi Machi kwa asilimia 81. Hii ni kutokana na vuta nikuvute katika eno la Gatuna mpakani, na kuwaathiri wasafiri pamoja na wafanyibiashara.

    Mnamo mwezi Februari mwaka huu, Rwanda ilifunga baadhi ya sehemu zake mpakani na kulemaza shughuli za biashara. Kulingana na Benki ya Uganda, mapato kutoka Rwanda yalipungua kutoka doa milioni 14.51 mwezi Februari mwaka huu hadi dola milioni 2.64 mwezi Machi. Haya ni mapato ya chini zaidi kuwahi kutoka Rwanda tangu mwaka wa 2006. Hadi sasa biashara bado imelemezwa kutokana na Rwanda kufunga mipaka yake ili kuwazuai wafanyibiashara wa Uganda kufanya shughuli zao.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako