• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Balozi wa Jamhuri ya Kongo nchini China asema pendekezo la "Ukanda Mmoja, Njia Moja" limenufaisha nchi zinazojiunga nalo

    (GMT+08:00) 2019-05-20 19:18:41

    Balozi wa Jamhuri ya Kongo nchini China Bw. Daniel Owassa amesema mifano ya ushirikiano kati ya China na Afrika inaonyesha kuwa pendekezo la "Ukanda Mmoja, Njia Moja" ni zuri na lina ushawishi chanya, na washirika wanaweza kushirikiana badala ya kuathiriwa na wengine wasio na nia nzuri.

    Ikiwa ni sehemu ya mfululizo wa sherehe za maadhimisho ya Siku ya Ukombozi wa Afrika tarehe 25 mwezi huu, "Baraza la mitizamo ya China na Afrika" ambalo pia ni Mashindano ya kirafiki ya soka kati ya wanadiplomasia wa Afrika pamoja na watoto wao, na wanafunzi na walimu kutoka Beijing ya "Ukanda Mmoja, Njia Moja" yamefanyika mjini Beijing.

    Balozi Owassa amesema pendekezo hilo limeleta mafanikio mengi kwa nchi mbalimbali, kama vile kuanzisha maeneo ya viwanda, kujenga barabara, bandari na miundombinu mingine, na matokeo hayo yamechangia nchi yake na kuwanufaisha wenyeji.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako