• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Profesa wa chuo kikuu cha Yale asema Marekani inatakiwa kujifunza kutokana na historia

    (GMT+08:00) 2019-05-20 19:53:54

    Profesa Stephen Roach wa Chuo Kikuu cha Yale cha Marekani, amesema kitendo cha serikali ya Bw. Trump kuongeza ushuru dhidi ya bidhaa za China zinazouzwa Marekani kinafanana na sera ya kujilinda kibiashara iliyotekelezwa na Marekani katika miaka ya 30 ya karne iliyopita. Ameitaka serikali ya Trump kusimamisha uamuzi huo, na kujifunza kutokana na historia ili kuepusha kufanya tena makosa makubwa.

    Akiongea kwenye mahojiano na televisheni ya Bloomberg, Profesa Roach amesema, mwezi wa Mei mwaka 1930, wachumi zaidi ya elfu 1 walimwandikia barua aliyekuwa rais wa Marekani Bw. Herbert Hoover kumtaka asiidhinishe sheria ya ushuru ya Smoot Hawley, lakini alipuuza na kuisaini, na Marekani ilianza kutoza ushuru wa kiwango cha juu dhidi ya bidhaa zaidi ya elfu 20 kutoka nchi za nje.

    Hatua hiyo ilisababisha wenzi wakuu wa kibiashara wa Marekani kulipiza kisasi na kuanzisha vita vya kibiashara duniani. Wachumi wanaona utekelezaji wa sheria hiyo ulikuwa chanzo kikuu cha msukosuko wa kiuchumi wa miaka 30 ya karne iliyopita.

    Bw. Roach anaona uzoefu wa historia unatuambia kuwa Marekani inakabiliwa na hatari ya kufanya tena kosa kubwa. Kosa hilo linatokana na rais kutosikiliza mapendekezo ya wataalamu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako