• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • WTO laonya dhidi ya kupungua kwa kasi ya ongezeko la biashara duniani katika robo ya pili ya mwaka

    (GMT+08:00) 2019-05-21 09:55:21

    Shirika la Biashara Duniani (WTO) limetoa ripoti mpya ya mustakabali wa biashara ikisema, kasi ya ongezeko la biashara duniani katika robo ya pili mwaka huu, inakadiriwa kuendelea kupungua.

    Ripoti hiyo imesema, kiwango cha ustawi wa biashara duniani katika robo ya pili ya mwaka huu ni alama 96.3 ikimaanisha kuwa, ongezeko la biashara litakuwa chini kuliko ilivyotarajiwa. Kiwango hicho kinayofanana na kile cha robo ya kwanza ya mwaka huu, kimekuwa chini zaidi tangu mwezi wa Machi, mwaka 2010.

    Habari zinasema, kutokana na mvutano wa biashara ya kimataifa, Shirika hilo limepunguza matarajio ya ongezeko la biashara ya kimataifa kutoka asilimia 3.7 hadi asilimia 2.6.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako