• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Wataalamu waona China ina imani ya kutosha ya kukabiliana na migogoro ya biashara na Marekani

  (GMT+08:00) 2019-05-21 19:12:09

  Hivi karibuni, Marekani iliongeza ushuru kwa bidhaa za China ili kuilazimisha China kukubali masharti yasiyofaa kwenye mazungumzo ya uchumi na biashara. Wataalamu wa China wanaona kuwa migogoro ya biashara kati ya China na Marekani haitaathiri uchumi wa China, na China itaikabiliana migogoro hiyo kwa imani kubwa.

  Tokea mwaka jana, Marekani imeongeza ushuru kwa baadhi ya bidhaa za China zinazouzwa nchini humo, hatua ambayo imeathiri uendeshaji wa baadhi ya kampuni za China, na Kampuni inayotengeneza betri ya lithiamu ya mkoa wa Hubei ni moja kati ya kampuni hizo, naibu meneja mkuu wa kampuni hiyo Bw. Liu Qi anasema:

  "Hatua yetu ya kwanza ni kuongeza uwezo wetu wa ushindani, na tulitumia fedha nyingi katika uendelezaji na marekebisho ya teknolojia, kutengeneza bidhaa za aina mpya, ili kuongoza soko kwa kutumia bidhaa zetu. Na sasa tunakabiliwa kwa utulivu hatua nyingine ya Marekani ya kuongeza ushuru. Katika robo ya pili au ya tatu ya mwaka huu, timu yetu ya wasimamizi waandamizi watajitahidi kuokoa oda zilizopotea kwa njia ya kudhibiti gharama za bidhaa. Ndiyo maana hivi sasa tumekuwa na imani ya kutosha kukabiliana na athari mbaya zitakazotokea katika siku za baadaye."

  Naibu mkuu wa kudumu wa Idara ya utafiti wa uchumi wa jumla iliyo chini ya Kamati ya Maendeleo na MNageuzi ya China Bw. Wang Changlin anaona kuwa, migogoro kati ya China na Marekani haiathiri uchumi wa China kama ilivyotarajiwa, kwani maendeleo ya China yana mustakabali na injini kubwa. Anasema:

  "Migogoro ya biashara kati ya China na Marekani itatuathiri kiasi lakini si kama ilivyotarajiwa na watu. Tutaweza kukabiliana na changamoto hizo kwa kuchukua hatua kadhaa na kuonesha sifa ya mfumo wetu na soko letu kubwa la uchumi, na mustakabali mkubwa wa soko la ndani."

  Naibu mkurugenzi wa Idara ya makadirio ya uchumi kwenye Kituo cha habari cha China Bw. Wang Yuanhong anaona kuwa, hatua hiyo ya Marekani italeta athari kwa maendeleo ya uchumi ndani ya muda mfupi, lakini kutokana na mtizamo wa muda mrefu ujao, shinikizo kama hilo litasukuma mbele mchakato wa mageuzi na ufunguaji mlango wa China. Akisema:

  "Hatua zilizochukuliwa na Marekani zimehusisha sekta nyingi ambazo zitaathiri uzalishaji, ajira hata bei za bidhaa za China ndani ya muda mfupi ujao. Lakini tukivumilia hasara hizo za muda mfupi, tutaweza kuonesha kihalisi kazi ya utaratibu wa soko kwa kufanya uvumbuzi, ufunguaji mlango na mageuzi, ili kuonesha uhai wa soko, na kutimiza maendeleo yenye sifa bora, ambalo ni lengo tunalolitafutia. "

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako