• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kampuni zaidi ya 170 za viatu za Marekani zaandika barua ya pamoja kupinga serikali ya Marekani kuongeza ushuru kwa bidhaa za China

    (GMT+08:00) 2019-05-21 19:30:28
    Kampuni zaidi ya 170 za viatu za Marekani zimeandika barua ya pamoja kuitaka serikali ya Marekani kuondoa viatu vilivyoingizwa kutoka China katika orodha ya bidhaa zilizoongezwa ushuru na kusema kitendo cha kuongeza ushuru kitadhuru maslahi ya wateja wa Marekani na uchumi wa nchi hiyo.

    Barua hiyo imesainiwa na kampuni kubwa za kimataifa, kampuni zenye ukubwa wa kati na ndogo, pamoja na kampuni za utengenezaji na za kampuni za mauzo.

    Habari kutoka shirika la wafanyabiashara wa jumla na wa rejareja wa viatu, zinasema ongezeko la ushuru kwa viatu vilivyotengenezwa na China linaweza kusababisha wateja wa Marekani kulipa fedha za ziada dola za kimarekani bilioni saba kwa mwaka.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako