• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Marekani yatangaza kuahirisha marufuku dhidi ya kampuni ya Huawei kwa siku 90

    (GMT+08:00) 2019-05-21 19:32:53

    Wizara ya biashara ya Marekani imetoa taarifa kupitia tovuti yake ikisema, nchi hiyo itatoa kibali cha muda wa siku 90 kwa kampuni ya Huawei ya China na washirika wake. Taarifa hiyo imesema, mpango huo unalenga kutoa muda wa kufanya marekebisho kwa idara na makampuni husika.

    Ripoti kutoka shirika la habari la Ufaransa AFP zinasema ofisa wa serikali ya Marekani amesema kampuni ya Huawei na wenzi wake wa kibiashara wanahitaji muda wa kushughulikia software na masuala kadhaa ya wajibu wa mikataba. Lakini ripoti hiyo pia imesema, kuahirisha utekelezaji hakumaanishi kuondolewa kwa marufuku hiyo, bali ni kuipa kampuni ya Huawei na wenzi wake muda wa kuhakikisha wanaboresha mtandao unaoendeshwa na vifaa vyake, ili kufuata mikataba na makubaliano yaliyosainiwa Mei 16 mwaka 2019 na kabla.

    Mzinduzi wa kampuni ya Huawei Bw. Ren Zhengfei akihojiwa na vyombo vya habari vya China amesema, kibali cha muda wa siku 90 kinachotolewa na Marekani hakina maana kubwa kwao, jambo muhimu zaidi kwao ni kufanya vizuri mambo wanayoyamudu, lakini hawawezi kuamua shughuli za serikali ya Marekani.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako