• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais wa Tanzania awaamuru maofisa wa ngazi ya juu kutumia huduma za simu za kampuni inayomilikiwa na serikali

    (GMT+08:00) 2019-05-22 08:44:03

    Rais John Magufuli wa Tanzania amewaamuru maofisa wote wa ngazi ya juu wa serikali kutumia huduma za simu zinazotolewa na kampuni ya simu inayomilikiwa na serikali, TTCL.

    Akizungumza katika hafla iliyotangazwa moja kwa moja na Televisheni ya Taifa nchini humo TBC, rais Magufuli amewapa maofisa hao siku 30 kuanzia jana kuanza kutumia huduma za simu za TTCL, na kuongeza kuwa kufanya hivyo kutaongeza kipato cha kampuni hiyo.

    Tanzania ina kampuni binafsi kadhaa zinazotoa huduma za simu ikiwemo Airtel, Vodacom, Halotel na Tigo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako