• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Watu 50 wafariki na wengine 41 wajeruhiwa katika ajali kwenye machimbo ya madini kwa mwaka huu

    (GMT+08:00) 2019-05-22 08:44:45

    Watu 50 wamefariki na wengine 41 kujeruhiwa katika ajali zinazohusiana na uchimbaji wa madini kuanzia mwanzoni mwa mwaka huu nchini Rwanda.

    Katibu mkuu wa Mamlaka ya Uchunguzi ya Rwanda (RIB) Bw. Jeannot Ruhunga amesema, marehemu hao walijihusisha na uchimbaji haramu wa madini, na kwamba kampeni za kuongeza uelewa zimeanzishwa ili kuwaelimisha wananchi kuhusu vitendo vya kibinadamu vinavyoathiri mazingira.

    Bw. Ruhunga amewataka wananchi kutojihusisha na vitendo vinavyoweza kuharibu mazingira, ikiwemo uchimbaji haramu wa madini, kukata miti, kuchoma mkaa na kuvamia maeneo oevu yaliyotengwa na serikali, kwani vitendo hivyo ni sawa na uhalifu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako