• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Mwanzilishi wa Huawei ahojiwa na vyombo vya habari

  (GMT+08:00) 2019-05-22 09:46:41

  Mwanzilishi wa Kampuni ya Huawei ya China Bw. Ren Zhengfei jana akihojiwa na vyombo vya habari katika makao makuu ya kampuni hiyo mjini Shenzhen, amesema sekta ya teknolojia ya juu ya Huawei haitaathiriwa na vikwazo vya Marekani.

  Bw. Ren ameyashukuru mashirika ya Marekani kwa uungaji mkono na ushirikiano wao na Huawei. Amesema, "Nayashukuru sana mashirika ya Marekani. Katika miaka 30 iliyopita, mashirika hayo yameungana na Huawei katika mchakato wake wa maendeleo, na kutoa mchango wa dhati. Viwanda vya vipuri vya Marekani vimetusaidia sana, haswa katika wakati huu wa hatari."

  Wizara ya biashara ya Marekani imeweka Huawei na mashirika yake kwenye orodha nyeusi. Baadhi ya vyombo vya habari vina wasiwasi kuwa, hatua hiyo itaathiri utendaji wa Huawei. Bw. Ren amesema, "Hadi sasa kampuni za Marekani bado zinaishawishi serikali ya nchi hiyo kuacha vikwazo dhidi ya Huawei. Tunapaswa kufahamu kuwa kuna aina nne za vikwazo. Kampuni za Marekani zinatakiwa kutoa ombi kwa serikali yao kabla ya kuuza kitu chochote kwa Huawei. Lakini vikwazo hivyo havitaathiri sekta yetu ya teknolojia ya juu, haswa teknoljia ya 5G. Tuna uhakika kuwa kampuni nyingine haziwezi kufikia kiwango chetu katika miaka miwili au mitatu ijayo."

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako