• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Balozi wa Korea Kaskazini kwenye Umoja wa Mataifa akosoa Marekani kwa kushikilia meli ya mzigo

    (GMT+08:00) 2019-05-22 09:57:56

    Mwakilishi wa kudumu wa Korea Kaskazini kwenye Umoja wa Mataifa balozi Kim Song amekosoa Marekani kwa kushikilia meli ya mzigo ya nchi yake. Amesema Mei, 9, Marekani ilifanya "kitendo haramu na cha kukasirisha" cha kukamata meli ya mzigo ya Korea Kaskazini Wise Honest kwa kuilazimisha iende eneo lake huko Samoa kwa kutumia kisingizio cha vikwazo vya upande mmoja na ukiukaji wa sheria ya ndani ya Marekani. Ameongeza kuwa amekabidhi barua kwa katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres na kumwelezea kuhusu msimamo wao juu ya tukio hilo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako