• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yatoa msaada wa vifaa vya kilimo kwa Zimbabwe

    (GMT+08:00) 2019-05-22 19:10:35

    Wizara ya kilimo na vijiji ya China imeipatia wizara ya kilimo ya Zimbabwe msaada wa vitu na vifaa vya kilimo vyenye thamani ya dola za kimarekani laki 1.36.

    Msaada huo umetolewa mjini Harare, na vifaa hivyo vinatumiwa kwa pamoja na wizara ya kilimo ya Zimbabwe na wataalamu wa kilimo wa China wanaoisaidia Zimbabwe katika sekta ya utafiti wa kilimo, uzalishaji na mafunzo ya ufundi wa kilimo.

    Balozi wa China nchini Zimbabwe Bw. Guo Shaochun amesema mchango huo unaonyesha ushirikiano kati ya China na Zimbabwe katika sekta ya kilimo, na katika miaka ya hivi karibuni timu ya wataalamu wa kilimo wanaoisaidia Zimbabwe wametoa mchango muhimu kwa maendeleo ya kilimo cha kisasa, na kutimiza kujitosheleza kwa chakula kwa Zimbabwe, na nchi hizo mbili zitaendelea kushirikiana katika sekta ya kilimo.

    Naibu waziri wa kilimo wa Zimbabwe Bw. Douglass Karoro amesifu mchango huo na kusema unasaidia kuongeza kiwango cha uzalishaji wa kilimo na uwezo wa utafiti wa Zimbabwe.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako