• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Baraza la mawaziri la Uganda lapitisha kuanzishwa kwa miji tisa

    (GMT+08:00) 2019-05-22 19:31:35

    Baraza la mawaziri la Uganda limepitisha kuanzishwa kwa majiji tisa kwenye sehemu mbalimbali nchini humo, ikiwa ni sehemu ya juhudi za kuboresha ujenzi wa miundo mbinu mijini.

    Mawaziri wamekubaliana kuwa majiji tisa yanatakiwa kuanzishwa, majiji hayo yatakuwa ni Mbarara, Hoima na Fort Portal magharibi mwa Uganda, Jinja na Mbale mashariki, Entebbe katika sehemu ya katikati, Gulu, Lira na Arua kaskazini ambayo yataanzishwa kati ya mwaka 2020 na mwaka 2022.

    Taarifa iliyotolewa na kituo cha habari inasema matokeo ya mpango huo yanatarajiwa kuongeza mapato na uhamishaji wa fedha wa serikali, na kuongeza viwango vya ajira. Kwa sasa Uganda ina jiji moja tu katikati ya nchi hiyo, lenye watu zaidi ya milioni 1.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako