• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mtaalamu wa Marekani asema serikali ya Trump ni tishio kubwa zaidi kwa utawala wa sheria duniani

    (GMT+08:00) 2019-05-22 19:44:47

    Mtaalamu wa Marekani Bw. Jeffrey Sachs leo amehojiwa na vyombo vya habari vya China, na kukosoa kitendo cha serikali ya Marekani cha kuiwekea vizuizi kampuni ya vifaa vya mawasiliano ya Huawei ya China, ambacho ni hatua ya hatari.

    Bw. Sachs amesema China si adui wa Marekani, bali ni nchi inayojaribu kuboresha maisha ya wananchi wake kupitia elimu, biashara, uwekezaji kwenye miundombinu na kurekebisha teknolojia. Lakini kitendo cha hivi sasa cha Bw. Trump kina lengo la kuzuia maendeleo ya China. Hali halisi ni kwamba China inajitahidi kunakili, kununua, kuiga na kuboreshsha teknolojia ya nchi za Ulaya na Marekani kupitia uvumbuzi wake wa ndani, si kitendo cha "kuiba" teknolojia kama Marekani inavyosema.

    Ameongeza kuwa vita vya biashara dhidi ya China haiweza kutatua matatizo ya kiuchumi ya Marekani, na kushirikiana na China ndiyo njia mwafaka itakayoinufaisha Marekani.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako