• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wizara ya mambo ya nje ya China yapendekeza wanasiasa wa Marekani wawe na nia ya afya kwa juhudi za nchi nyingine za kusaidia Afrika

    (GMT+08:00) 2019-05-22 19:54:23

    Msemaji wa wizara ya mambo ya nje wa China Bw. Lu Kang amesema kama Marekani inafuatilia nchi zinazoendelea, ni bora itoe msaada, na kama haiwezi kufanya hivyo basi bora iwe na moyo wa kuvumilia juhudi za nchi nyingine kusaidia maendeleo ya Afrika.

    Habari zimesema mbunge wa baraza la chini la bunge la Marekani Bw. Brad Sherman amehimiza hoja ya mtego wa madeni wa China ili kuzifanya nchi nyingine kukwepa mtego wa madeni wa China.

    Bw. Lu amesema kwa mfano wa Afrika, rais Hage Geingob wa Namibia amewaambia waandishi wa habari, kwa kweli mikopo ya China inachukua asilimia 2.6 ya mikopo yote ya serikali ya Namibia, na mingi haina riba, na makubaliano yaliyofikiwa na pande hizo mbili kwa haki, bila ya masharti yoyote ya siasa. Pia amesema uwekezaji wa China kwa Namibia si kama tu unahusisha miradi mikubwa ya uwanja wa ndege, na barabara, bali pia sekta ya elimu, matibabu na kilimo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako