• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • IFAD yasaidia miradi Arumeru

    (GMT+08:00) 2019-05-22 20:59:07
    Halmashauri ya Meru wilayani Arumeru, imetekeleza miradi yenye thamani ya shilingi bilioni 1.6, kupitia mfuko wa Kimataifa wa maendeleo ya Kilimo (IFAD), kwa ushirikiano na Benki ya Maendeleo ya Afrika (AFDB). Akitoa taarifa kwa rais wa IFAD, Gilbert Haungbo, Mkuu wa Wilaya ya Arumeru, Jerry Muro, alisema miradi hiyo imetekelezwa kufuatia taasisi hizo za kimataifa, kuingia ubia na Serikali ya Tanzaniamwaka wa 2011.

    Miradi hiyo imetekelezwa kupitia programu ya miundombinu ya masoko,uongezaji thamani na huduma za fedha vijijini (MIVARF). Akiwa katika kiwanda cha kusindika maziwa cha The Grand Deman, kilichopo Leganga emeo la Usa River wilayani Arumeru, Rais huyo wa IFAD alielezwa na Muro kuwa, miradi hiyo imetekelezwa kwa lengo la kuimarisha uchumi wa nchi. Miradi mingine ni ukarabati wa ghala lenye uwezo wa kuhifadhi tani 300 katika kijiji ca King'ori.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako