• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wamiliki wa 14 Riverside kufidiwa

    (GMT+08:00) 2019-05-22 21:00:19
    Wamiliki wa jengo la 14 Riverside mtaani Westlands, Naiorbiwanatarajia kulipwa shilingi milioni 400 kama bima kutokana na hasara waliyopata baada ya shambulizi la kigaidila Januari 15, ambapo watu zaidi ya 21 walipoteza maisha yao.

    Fidia hiyo inahusiana na uharibifu wa mali na kupoteza kwa mapato katika jumba lote la 14 Riverside, ikiwemo hoteli ya DusitD2 Hotel.

    Wamiliki wa jumba hilo walikuwa wamechukua bima dhidi ya ugaidi na kampuni ya GA Insurance. 14 Riverside huwa na biashara tofauti zikiwemo ni pamoja na biashara rejareja, vyombo vya habari na biashara zingine ikiwemo hoteli ya DusitD2. Hoteli hiyo ilitarajiwa kufunguliwa mapema Juni, lakini tarehe ya kufunguliwa imesongeshwa hadi Agosti, kulingana na habari zilizoko katika tovuti yake.

    Hata hivyo, hoteli hiyo bado inapokea maombi kutoka kwa wateja kuwahifadhia vyumba au kumbi.

    Kundi la kigaidi la al-Shabaab lilikiri kuhusika katika shambulizi hilo, ambalo pia liliacha baadhi ya wateja wakiwa na majeraha.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako