• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Ethiopia yakaribisha uwekezaji kutoka kampuni za teknolojia ya madawa za China

    (GMT+08:00) 2019-05-23 08:26:23

    Serikali ya Ethiopia imezitaka kampuni za teknolojia ya madawa kutoka China kutafiti fursa nyingi za uwekezaji zilizopo nchini Ethiopia, hususan katika uwekezaji wa sekta ya madawa.

    Wito huo umetolewa na waziri wa mambo ya nje wa Ethiopia Aklilu Hailemichael wakati alipokutana na wawakilishi wa kampuni za madawa za China katika mji mkuu wa Ethiopia, Addis Ababa hapo jana. Amesema wizara yake kwa kushirikiana na wizara ya afya na taasisi nyingine husika zitaunga mkono kampuni za China kuwekeza katika sekta ya madawa nchini humo.

    Ujumbe wa China umesema vifaa vya kisasa vya matibabu vya China vitasaidia juhudi za Ethiopia za kuboresha sekta yake ya afya, hususan umuhimu wa matibabu ya saratani na magonjwa mengine makubwa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako