• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Bunge la Afrika Kusini lamchagua Cyril Ramaphosa kuwa Rais wa nchi hiyo

    (GMT+08:00) 2019-05-23 08:35:24

    Bunge la Afrika Kusini limemchagua mgombea kutoka chama tawala cha ANC Bw. Cyril Ramaphosa kuwa rais wa nchi hiyo.

    Wabunge wapya wa Afrika Kusini walioapishwa jana Jumatano mjini Cape town, walipiga kura na kumchagua Bw. Cyril Ramaphosa kuwa rais mpya wa nchi hiyo kwa muhula wa miaka mitano.

    Bw. Cyril Ramaphosa ataapishwa rasmi Jumamosi ijayo mjini Pretoria.

    Baada ya kuchaguliwa, Bw. Ramaphosa amesema atapigania maslahi ya wananchi wote wa Afrika Kusini, na sio kuwahudumia watu wachache, na kujenga Afrika Kusini kwenye msingi wa kutetea haki za jamii.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako