• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Afrika mashariki kuzindua mazoezi ya kujiandaa kwa milipuko ya magonjwa ya kuambukiza

    (GMT+08:00) 2019-05-23 08:35:45

    Jumuiya ya Afrika Mashariki EAC inapanga kuzindua mazoezi ya kuvuka mipaka ya kujiandaa kwa milipuko ya magonjwa ya kuambukiza huko Namanga, mji wa mpakani kati ya Kenya na Tanzania mnamo mwezi Juni.

    Jumuiya hiyo imesema mazoezi hayo yanayotarajiwa kufanyika kuanzia Juni 11 hadi 14, yanalenga kuimarisha utayari na hatua za kukabiliana na milipuko ya magonjwa ya kuambukiza kwenye kanda hiyo kwa kutumia mkakati wa pamoja wa "One Health Approach".

    Katika miaka ya nyuma, Jumuiya ya Afrika Mashariki imeshuhudia milipuko ya magonjwa ya kuambukiza kama Ebola, homa ya Bonge la Ufa, Marburg, homa ya Crimea-Kongo, Kipindupindu, polio na tauni.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako