• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Ofisa wa Umoja wa Mataifa asema hali ya kibinadamu ya Somalia inazorota

    (GMT+08:00) 2019-05-23 08:43:44

    Msaidizi wa katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa anayeshughulikia mambo ya kibinadamu Bibi. Ursula Mueller ameonya kuwa hali ya kibinadamu ya Somalia inazorota kutokana na kuenea kwa ukame kutoka maeneo ya kaskazini hadi katikati ya nchi hiyo.

    Akizungumza kwenye kikao cha Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, Bi. Mueller amesema mapambano na vurugu zinazoendelea, pamoja na majanga yanayotokana na mabadiliko ya hali ya hewa zinalazimisha nchi hiyo kuhitaji misaada ya kibinadamu.

    Wakati huo huo, mratibu wa kisiasa wa ujumbe wa kudumu wa China kwenye Umoja wa Mataifa Bw. Yao Shaojun amesema, jumuiya ya kimataifa inapaswa kuiunga mkono Somalia katika ujenzi wa uwezo wa kulinda usalama na maendeleo ya kibinadamu, kiuchumi na kijamii.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako