• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • SOKA: Ligi kuu Tanzania bara, Yanga yaipiga Mbeya City, Makambo aaga mashabiki

  (GMT+08:00) 2019-05-23 08:57:20
  Ligi kuu Tanzania Bara imeendelea jana kwa mchezo kati ya Yanga na Mbeya City uliopigwa uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.

  Yanga imeibuka na ushindi wa goli 1-0 lililofungwa na mchezaji wa kimataifa kutoka DRC Heritier Makambo dakika ya 26 ya mchezo. Yanga sasa wanafikisha alama 86 baada ya kucheza michezo 37 wakizidiwa alama 5 na mabingwa wa ligi hiyo Simba.

  Wakati huo huo, Makambo ametumia fursa ya mchezo huo kuwaaga mashabiki wa Yanga na kueleza anaondoka Yanga mwishoni mwa msimu huu na kuna mengi ambayo atayakumbuka katika kikosi cha timu hiyo kwa muda wa mwaka mmoja ambao ameishi licha ya changamoto mbalimbali.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako