• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • VOLIBOLI: Kufuzu Voliboli ya wanawake Afrika-Kenya watumia wembe ule ule kuwanyoa Uganda

  (GMT+08:00) 2019-05-23 08:57:50
  Kenya ilitolewa kijasho na Uganda katika seti ya kwanza kabla ya kuwanyoa seti 3-0 katika mechi ya mwisho ya ukanda wa tano na kufuzu kushiriki voliboli ya wanawake kwenye mashindano ya bara Afrika (All-African Games) katika ukumbi wa Lugogo jijini Kampala.

  Malkia Strikers ilikuwa alama moja tu mbele ya Uganda 21-20 katika seti ya kwanza kabla ya kushinda wenyeji hao 25-20. Baada ya kubabaishwa katika seti ya kwanza, Kenya ilirejea katika seti mbili zilizofuata kwa nguvu zaidi na kuzinyakua 25-17, 25-16, mtawalia.

  Kenya sasa itaenda nchini Mororcco katika mashindano ya voliboli ya wanawake Afrika.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako