• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • SOKA: FIFA wabariki Qatar kuwa mwenyeji wa michuano ya Kombe la Dunia mwaka 2022 kwa timu 32 sio 48

  (GMT+08:00) 2019-05-23 08:58:34
  Shirikisho la soka duniani (FIFA) limetangaza kuwa imelazimika kuacha michuano ya kombe la dunia mwaka 2022 itakayofanyika nchini Qatar kuwa na timu 32 na sio 48 kama ambavyo ilikuwa inatarajiwa awali, taarifa hizo rasmi zitatolewa Juni 5 mwaka huu katika mkutano wa FIFA mjini Paris Ufaransa.

  Inaelezwa kuwa Qatar wamekuwa wakijipanga kuwa wenyeji wa timu 32 toka 2010 na hata maandalizi yao yalikuwa yanalenga kutumia viwanja nane vilivyoandaliwa tayari, hivyo kwa miaka mitatu iliyosalia Qatar hawezi kumudu ongezeko la timu kutoka 32 yaliokuwa matarajio yao hadi 48.

  Hata hivyo wazo la timu 48 linabakia kuwa kama wazo litakaloanza kufanya kazi rasmi 2026 katika fainali za Kombe la Dunia litakalokuwa na wenyeji watatu United States, Canada na Mexico, sababu za kisiasa ndio zimeleta utata kwa Qatar kukubali ongezeko la timu na kuwa mwenyeji kwa ushirikiano na mataifa jirani.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako