• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kiongozi wa chama cha upinzani cha Malawi aongoza kwenye uchaguzi mkuu

    (GMT+08:00) 2019-05-23 09:14:33

    Tume ya uchaguzi ya Malawi jana imesema, kiongozi wa chama cha upinzani anaongoza kwenye uchaguzi mkuu uliofanyika tarehe 21 Mei.

    Mwenyekiti wa tume ya uchaguzi ya Malawi Jane Ansah amesema, kiongozi wa chama cha MCP Lazarus Chakwera amepata kura 533,217, ikiwa ni asilimia 37.65 ya kura zilizohesabiwa kutoka vituo 1,784 kati ya vituo vyote 5,002 vilivyotumika katika kupiga kura.

    Bw. Lazarus anafuatiwa na rais wa sasa Peter Mutharika ambaye amepata kura 524,247, huku makamu wa rais Saulos Chilima akipata kura 293,978.

    Matokeo ya mwisho yanatarajiwa kutangazwa ndani ya siku 8 baada ya upigaji kura.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako