• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mawaziri wa nchi za nje wa SCO waunga mkono msimamo wa China juu ya mgogoro wa kibiashara kati ya China na Marekani

    (GMT+08:00) 2019-05-23 09:25:41

    Waziri wa mambo ya nje wa China Bw. Wang Yi amesema, mawaziri mambo ya nje wa nchi wanachama wa Shirika la Ushirikiano wa Shanghai SCO, wanaelewa na kuunga mkono msimamo wa China juu ya mgogoro wa kibiashara kati ya China na Marekani.

    Akizungumza na waandishi wa habari kando ya mkutano wa baraza la mawaziri wa mambo ya nje wa Shirika la Ushirikano wa Shanghai mjini Bishkek, Kyrgyzstan, Bw. Wang amesema amewafahamisha wenzake kuwa mazugumzo ya kibiashara kati ya China na Marekani yanazuiliwa na Marekani kwa kutopenda kutatua ufuatiliaji wa China. Amesisitiza kuwa hatua zinazochukuliwa na China si kama tu zinalinda maslahi yake halali, bali pia zinalinda kanuni ya mahusiano ya kimataifa na mfumo wa biashara huria.

    Ameongeza kuwa kuiwekea vikwazo kampuni ya China ya Huawei bila sababu yoyote ni kitendo cha ukandamizaji wa kiuchumi cha Marekani, ambacho kinajaribu kuzuia maendeleo ya China, na hakitakubaliwa na jumuiya ya kimataifa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako