• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • China yatoa mwito wa kushikilia suluhu ya nchi mbili kwenye mgogoro kati ya Palestina na Israel

  (GMT+08:00) 2019-05-23 10:47:55

  Mwakilishi maalum wa China kwenye Umoja wa Mataifa Balozi Ma Zhaoxu ametoa mwito wa kushikilia suluhu ya nchi mbili katika kutatua mgogoro kati ya Palestina na Israel. Amesema jumuiya ya kimataifa inatakiwa kufanya kazi katika msingi wa kuheshimu Pendekezo la Amani la Uarabu, kanuni za kurudisha ardhi kwa amani na maazimio husika ya Baraza la Usalama ili kuhimiza utatuzi wa suala la Palestina kwa mtazamo wa kuanzisha taifa la Palestina lenye mamlaka kamili katika msingi wa mipaka iliyowekwa mwaka 1967 na Jerusalem Mashariki ikiwa mji mkuu. Ameongeza kuwa kwa kufanya hivyo utatuzi wa suala hilo utakuwa wa haki na kudumu na pia utakubaliwa na jumuiya ya kimataifa.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako