Msemaji wa jeshi linalounga mkono serikali ya Yemen katika pwani ya magharibi mwa nchi hiyo Waddah Dubaish amethibitisha kuwa, wawakilishi wa serikali ya Yemen kwenye Kamati ya Uratibu wa Urejeshaji Mpya RCC katika mji wa bandari wa Hodeidah wamesitisha mikutano yao na kiongozi wa kamati hiyo, Michael Lollesgard. Amesema sababu ni kuwa kikosi cha serikali hakiruhusiwi kuingia katika bandari za Hodeidah kusimamia kujitoa kwa kundi la Houthi. Pande hasimu nchini Yemen zilifikia makubaliano chini ya Umoja wa Mataifa mwezi Disemba mwaka jana mjini Stockholm, ambayo yalihusisha kusitishwa vita mjini Hodeidah na kuanzishwa kwa kamati ya RCC ili kusimamia kuondoka kwa vikosi vya serikali na kundi la waasi katika mji huo.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |