• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Botswana na China zafanya mkutano wa uchumi kuhusu kuimarisha ushirikiano

    (GMT+08:00) 2019-05-23 19:23:55

    Botswana na China zimefanya mkutano wa uchumi na biashara mjini Gaborone ili kutafuta fursa zaidi za kuhimiza ushirikiano kati ya pande mbili.

    Maofisa waandamizi na wanadiplomasia wa Botswana na China wamehudhuria mkutano wa kwanza wa kamati ya pamoja ya uchumi, biashara, uwekezaji na ushirikiano wa kiufundi uliofanyika mjini Gaborone.

    Naibu waziri wa biashara wa China Bw. Qian Keming, amesema mkutano huo utaimarisha ushirikiano wa muda mrefu kati ya China na Botswana, na China iko tayari kushiriki kikamilifu kwenye kuimarisha ushirikiano huo ili kuleta matokeo yanayoonekana kwa watu wa nchi hizo mbili.

    Kaimu waziri wa mambo ya kimataifa na ushirikiano wa Botswana Bw. Nonofo Molefhi, amesema Botswana inaichukulia China kama mshirika wa kimkakati wa maendeleo, na inatumai kuona ushiriki zaidi wa China kwenye kufanya uchumi wa Botswana uwe na vyanzo mbalimbali.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako