• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Kongamano la kimataifa la teknolojia ya televisheni la Beijing la mwaka 2019 lafanyika hapa Beijing

  (GMT+08:00) 2019-05-23 20:29:55

  Kongamano la kimataifa la teknolojia ya televisheni la Beijing la mwaka 2019 linaloandaliwa kituo kikuu cha redio na televisheni cha China CMG limefanyika hapa Beijing. Wasomi, wataalamu na wadau zaidi ya 500 kutoka sekta za vyombo vya habari, mawasiliano ya simu, teknolojia ya habari wameshiriki katika kongamano hilo.

  Katika ufunguzi wa kongamano hilo, kituo cha usimamizi wa teknolojia ya televisheni ya CCTV cha CMG kimesaini makubaliano ya ushirikiano wa kimkakati na chuo kikuu cha Jiao Tong cha Shanghai, ili kujenga kwa pamoja maabara ya video ya kiwango cha juu na vifaa vya vyombo vya habari vya akili bandia.

  Kwa mujibu wa makubaliano hayo, pande hizo mbili zitafanya utafiti wa video ya kiwango cha juu na teknolojia ya akili bandia na kuhimiza uvumbuzi.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako