• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Mkutano wa tano wa wakuu wa mikoa na majimbo kati ya China na Marekani wafunguliwa

  (GMT+08:00) 2019-05-23 20:35:27

  Mkutano wa tano wa wakuu wa mikoa na majimbo kati ya China na Marekani umefunguliwa mjini Lexington, Kentucky, Marekani. Washiriki wa mkutano huo wamesema, katika mustakabali ambao uhusiano kati ya nchi hizo mbili unakabiliwa na hali ngumu, kuna umuhimu mkubwa wa kuimarisha mawasiliano na ushirikiano kati ya mikoa na majimbo.

  Watu 400 hivi wakiwemo wakuu, manaibu wakuu na meya kutoka mikoa ya Gansu, Jiangxi, Shaanxi na mji wa Chongqing, magavana na naibu magavana wa majimbo ya Kentucky, Tennessee, Washington, Colorado na Michigan pamoja na wadau wa uchumi na biashara wa nchi hizo mbili wamehudhuria mkutano huo, na kujadili ajenda kuhusu elimu na utamaduni, utengenezaji wa teknolojia ya hali ya juu, ujenzi na uwekezaji kwenye miundombinu na biashara za kielektroniki na kuvuka mipaka.

  Balozi wa China nchini Marekani Bw. Cui Tiankai amesema, ushirikiano wa kimajimbo na kimikoa ni sehemu muhimu ya uhusiano kati ya China na Marekani, ambao pia unatakiwa kuwa ongezeko jipya la ushirikiano kati ya nchi hizo mbili katika siku za baadaye.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako