• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya-Mfumuko wa bei kufika asilimia 11.7 kutokana na mvua isiyotosha

    (GMT+08:00) 2019-05-23 20:55:31

    Kiwango cha mfumuko wa bei cha Kenya huenda kikafika asilimia 11 kufikia mwezi Disemba,labda kuwe na mvua ya kutosha.

    Haya yalisemwa na Ofisi ya Bajeti ya Bunge.

    Hii inamaanisha kuwa wakenya wanafaa kujiandaa kwa wakati mgumu huku bei za bidhaa muhimu zikipanda.

    Kiwango cha mfumuko cha asilimia 11 kimezidi malengo ya serikali ya kiwango cha juu cha asilimia 7.5 na cha chini cha asilimia 2.5.

    Kulingana na Ofisi ya Bajeti ya Bunge,japokuwa hali nzuri ya hewa imetajwa kuwa kichocheo kikuu cha ukuaji wa uchumi mwkaa 2019,utendaji mbaya wa mvua katika kipindi cha mvua cha mwezi Machi-May huenda ukaathiri uzalishaji wa chakula nchini,na hatimaye kuporomoka kwa uchumi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako