• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Baraza la Wawakilishi Tanzania lataka wawekezaji wageni kulazimishwa kuajiri wafanyakaza wazalendo

    (GMT+08:00) 2019-05-23 20:57:13

    Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi nchini Tanzania wameitaka serikali kutayarisha sera ya ajira ambayo itakuwa mwongozo na kuwabana wawekezaji wa kigeni na kuwalazimisha kuajiri wafanyakazi wazalendo nchini humo.

    Mwakilishi wa Shauri Moyo, Hamza Hassan Juma, aliyasema hayo wakati akichangia bajeti ya makadirio mapato na matumizi ya Wizara ya Habari, Utamaduni, Utalii na Mambo ya Kale kwa mwaka 2019-2020.

    Juma alisema hakuna sera ya ajira ambayo inawaelekeza wawekezaji wa nje kuajiri wafanyakazi wazalendo katika sekta mbalimbali ikiwamo hoteli za kitalii.

    Alisema hoteli nyingi za kitalii zimeajiri wafanyakazi wa kigeni kwa visingizio mbalimbali ikiwamo hakuna wafanyakazi wazalendo wenye sifa.

    Alisema njia pekee ya kuwabana ni kuweka sheria madhubuti na kuhakikisha wafanyakazi wazalendo wanapata ajira.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako