• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Uganda-URA ina miezi miwili kukusanya Shs1.6 trilioni

    (GMT+08:00) 2019-05-23 20:57:32

    Mamlaka ya mapato Uganda (URA) imebakiza wiki tano kukusanya Shs1.6 trilioni (asilimia 10) kabla ya mwaka wa fedha 2018/19 kuisha.

    URA ina malengo ya kukusanya Shs16.3 trilioni kabla ya mwaka wa fedha 2018/19 kuisha laikini,kulingana na maelezo,kufikia sasa imekusanya Shs14.7 trilioni, na kuacha upungufu wa Shs1.6 trilioni, ambayo URA inafaa kukusanya kabla ya mwisho wa mwezi Juni.

    Akizungumza wakati wa utiaji saini ya ushirikiano kati ya URA na Airtel wa uzinduzi wa jukwaa jipya la ulipaji kodi kwa wafanyabiashara wadogo na wa kati,mjini Nakawa,Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Uganda,Bi Doris Akol alisema bado kuna asilimia 10 ambayo haijakusanyawa lakini juhudi zinafanywa ili ikusanywe kabla ya mwisho wa mwezi Juni.

    Bi Akol alisema ubia kati ya URA na Airtel ni mojawapo ya mipango mingi ambayo imeanzishwa ili kurahisisha ukusanyaji wa ushuru pamoja na kuisadia URA kufikia malengo yake.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako