Waziri Mkuu wa Tanzania Kassim Majaliwa amesema kuwa serikali inafanyia kazi mipango inayolenga kuwawezesha watanzania wanaoishi nje ya nchi kushiriki kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka 2020.
Akizungumza katika kikao cha bunge mjini Dodoma jana, Bw. Majaliwa amesema serikali iko kwenye mchakato wa kufahamu idadi kamili ya Watanzania wanaoishi nje ya nchi na wanaoweza kupiga kura katika uchaguzi wa Bunge na rais utakaofanyika Oktoba mwaka ujao.
Amesema mchakato huo pia utawezesha kutambua watanzania wanaoishi nje ya nchi ambao wana vitambulisho vya uraia na shughuli wanazofanya katika nchi hizo.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |