• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya yakana kuwa na mvutano wa kidiplomasia na Somalia

    (GMT+08:00) 2019-05-24 08:46:03

    Kenya imekana kuwa na mvutano wa kidiplomasia na nchi jirani ya Somalia.

    Katibu wa kudumu wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Kenya Machari Kamau amesema jijini Nairobi kuwa, Kenya daima imekuwa ikiwawezesha raia wa Somalia wanaoishi nchini Kenya, na kwamba Somalia inatakiwa kuheshimu mamlaka ya ardhi ya Kenya huku nchi hiyo nayo ikiheshimu kuwa kuna mahitaji kadhaa ambayo inayapata kutoka Somalia.

    Mapema wiki hii, maofisa watatu wa serikali ya Somalia wakiwa na hati za kusafiria za kibalozi walikataliwa kuingia nchini Kenya kupitia Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta. Kamau amesema, tukio hilo halimaanishi kuwa kuna uhusiano mbaya kati ya nchi hizo mbili, bali ni suala la uhamiaji.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako