• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Umoja wa Mataifa waunga mkono kazi zisichochafua mazingira Afrika Mashariki ili kuboresha mazingira endelevu

    (GMT+08:00) 2019-05-24 08:46:26

    Shirika la Kazi la Umoja wa Mataifa (ILO) limesema kuwa litaunga mkono ajira za kijani katika kanda ya Afrika Mashariki ili kuboresha mazingira endelevu.

    Mkurugenzi wa Ofisi ya Shirika hilo kwa nchi za Kenya, Tanzania, Burundi, Rwanda, na Uganda Bw. Wellington Chibebe amesema jijini Nairobi kuwa, kazi hizo zitawezesha eneo hilo kuchukua nafasi kubwa katika kukabiliana na athari za tabianchi. Amesema ILO itazisaidia nchi za Afrika Mashariki kukarabati sera zao za viwanda, mabadiliko ya tabianchi na kuboresha kazi za kijani kutokana na mapendekezo ya Shirikia hilo ili kuhakikisha zinatimiza mazingira endelevu.

    Chibebe amesema, kwa sera zilizo sahihi, Afrika Mashariki inaweza kuhamia kwenye uchumi wa kijani bila kuvuruga sana maisha ya watu wake. Ameongeza kuwa eneo hilo linaathirika zaidi na mabadiliko ya tabianchi kwa kuwa kiasi kikubwa cha watu wake wanategemea maliasili kujikimu kimaisha.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako